News
Loading...

SMS ZA KUCHEKESHA EP 01

 

 

Phone call✔

Phone call
gal: hellow
Boy: sweety mambo vipi?
Girl: poa
Boy: utakuwa free weekend? nilikuwa nataka uje nyumbani
Girl: oh sorry ctoweza kuja sababu kuna haruc ya aunt yangu
Boy: kama ni hivyo sawa nilikuwa nataka nikufanyie sapraiz nimekununulia IPHONE 7.
Girl: oh ucjal ntakuja na hata ntalala huko huko Boy: na haruc je?
Girl: nilikuwa nakutania
Boy: hata mi nilikuwa nakutania

Hili nalo neno kwa wavulana✔

Demu wako anakuja kwako kasuka nywele za 30,000 na hujampa hata mia,we unakalia kusema waooo waoooo kama king'ora cha ambulance.
Shauri yako we endelea kusema waoooo waooo na atakuwa wao kweli.

Vituko vinavyoandikwa kwenye daladala✔

.Huwa naenjoy sana kusoma yaliyoandikwa nyuma ya daladala hasa ninapokuwa kwenye foleni. Misemo maarufu
ya kwenye daladala.
1.Yatima hadeki
2.Utamu wa chips mimba
3.Ukitaka kujua ugumu wa kudai kopesha ukweni
4. Usiyempenda kaja
5. Kobe hapimwi joto
6. Acha kazi uone kaz kupata kaz
7. Ukichezea koki utalowa
8. Heshima pesa kipara kovu tu!
9. Mtumbwi hauna saitmira.
9. Silaha pesa bastola mzigo
10. Hata uoge mjini huendi
11. Chezea mshahara usichezee kazi.
12. Ukiona manyoya ujue kishaliwa
13. Ikisimama Panda
14. Pombe pombe tuu kunywea bar mbwebwe
15. Njia ya chooni haioti nyasi
16. Likizo ya maskini ugonjwa
17. When i grow up i want to be a scania
18. Hata bibi alikuwa binti
19. Kisigino hakikai mbele
20. Kama mapenz pesa kaolewe na benki
21. Hata barabara ina matuta lakin huwez panda viazi
22. Mavi hayana miba lakin ukikanyaga lazma uchechemee
23. Paka haishi kwa msela
24. Ukipendwa ujue kuna boya kaachwa
25. NIPO NIPO KWANZA
26. Mchana nzi ucku mbu
27. Ucmshangae funza kukata viuno ndio mwendo wake
28. Kama umelipenda(gari) bonyeza nyota liwe lako
29. Supermarket hawauzi mkaa
30. We nisubiri mi nakungoja.
31. Zetu dagaa kuku tamaa
32. Hata uwe na heshima vipi huwezi kumpokea askari bunduki


Share on Google Plus

About Sua Cerebrity

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 comments :