News
Loading...

19 universities and programs that you are not allowed to apply 2017/2018



 VYUO NA PROGRAMU ZILIZOZUILIWA KUDAHILI WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kuuarifu umma kuwa, mwezi Septemba na Oktoba mwaka 2016 ilifanya uhakiki wa vyuo vyote vya elimu ya juu nchini ili kuhakiki ubora wa elimu inayotolewa vyuoni. Ripoti ya uhakiki ilionesha mapungufu kadhaa katika baadhi vyuo. Kwa sababu hiyo, Tume imesitisha udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18 kwa vyuo vifuatavyo:

1.    Eckenforde Tanga University
2.    Jomo Kenyatta University, Arusha
3.    Kenyatta University, Arusha
4.    United African University of Tanzania
5.    International Medical and Technological University (IMTU)
6.    University of Bagamoyo
7.    St. Francis University College of Health and Allied Sciences
8.    Archibishop James University College
9.    Archibishop Mihayo University College
10.Cardinal Rugambwa Memorial University College
11.Kampala International University Dsm College
12. Marian University College
13.St. Johns University of Tanzania Msalato Centre
14.St. Johns University of Tanzania, Marks Centre
15.St. Joseph University College of Engineering and Technology
16.Teofilo Kisanji University
17.Teofilo Kisanji University Tabora Centre
18.Tumaini University, Mbeya Centre
19.Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMCo)
2.0 Aidha, kutokana na mapungufu katika vyuo mbalimbali imeamriwa kwamba jumla ya programu 75 kutoka vyuo 22 nchini zimesitishwa kudahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18. Kuona Programu ambazo zimesitishwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/18 tafadhali bonyeza hapa. 
3.0 Aidha Tume inapenda kusisitiza kwamba, uamuzi huu hautawahusu wanafunzi wanaondelea na masomo katika programu na vyuo husika
.

Imetolewa na:

Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji

24 Julai 2017 
Share on Google Plus

About Sua Cerebrity

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :

Post a Comment